Thursday , 10th Apr , 2014

Rapa kutoka nchini Kenya, Jua Cali amesema kuwa ana mpango wa kujiingiza katika tasnia ya filamu na kuanza kufanya uigizaji, kitu ambacho amekuwa akikitamani kwa muda mrefu sasa.

Jua Cali

Jua Cali amesema kuwa, katika miaka mitano ijayo anajiona katika nafasi ya staa mkubwa kabisa wa filamu, huku taarifa zikiweka wazi kuwa, mapenzi yake kwa fani ya uigizaji, yalianza zamani kabisa kabla hata ya kuanza kung'ara kupitia muziki.

Jua Cali amesema kuwa, anaamini kuwa atapiga hatua zaidi kupitia filamu kutokana na uwezo wake mkubwa katika suala zima la ubunifu ambao umuwezesha kufanya chochote katika sanaa.

Tags: