Tuesday , 9th Sep , 2014

Msanii Jose Chameleone, amepata msukumo wa aina yake kulekea onyesho lake ambalo atatoza kiingilio cha shilingi milioni 1 kwa kila kichwa, baada ya mfanyabiashara Katsha kutoka Afrika Kusini kununua tiketi 52 za onyesho hilo peke yake.

msanii wa muziki Jose Chameleone akiwa na mfanyabiashara Katsha wa Afrika Kusini

Chameleone akiwa nchini Afrika Kusini ambapo ndipo alipokutana na Katsha, alikabidhiwa kitita cha dola 20,000, zaidi ya shilingi milioni 52 za Uganda, kama kiingilio cha 'mnene' huyu katika shoo hii itakayofanyika mwezi wa 12.

Chameleone amesema kuwa, shoo hii ni kwa ajili ya kuwaita pamoja watu wenye uwezo kusapoti muziki wa Uganda, ambapo amemshukuru Katsha kwa sapoti kubwa aliyoonyesha.