John Legend
Kwa mujibu wa ratiba ya msanii huyu, Shoo hizi zitaanza rasmi tarehe 16 mpaka tarehe 23 mwezi Novemba, katika ziara hii ambayo imepatiwa jina “An Evening with John Legend: The All of Me Tour,”.
Hii inakuwa ni fursa nyingine kwa wapenzi wa burudani Afrika hususan kutoka ukanda wa kusini kupata burudni kali ya live kutoka kwa staa wa kimataifa, ambapo yeye binafsi amesema kuwa huwa anajisikia kuwa nyumbani anapokuwa Afrika.