Tuesday , 5th May , 2015

Staa wa muziki Joh Makini ameweka wazi kuwa, kupokelewa vizuri kwa kazi zake na mafanikio kwa ujumla ni kutokana na yeye kuishi maisha ya muziki huo kama uhalisia na kuifanya Hip Hop ya Tanzania ijulikane kimataifa.

msanii wa Hip hop wa kundi la Weusi Joh Makini

Joh Makini amesema kuwa lengo lake na la team nzima ya Weusi ni kuupatia thamani muziki huo wa Hip Hop, hatua ambayo inaonekana sasa kupitia rekodi, na shughuli mbalimbali za wasanii hao.