Friday , 25th Apr , 2014

Msanii wa muziki wa injili wa kimataifa, Joe Praize ambaye anafanya kazi zake huko Nigeria na Marekani, ametua nchini Tanzania kwaajili ya kazi zake za kimuziki, ikiwepo kushiriki kutoa burudani katika kanisa la Christ Ambassodors Dar es Salaam leo.

Joe Prize

Joe Praize ambaye ameweka wazi kuwa anafurahi sana kupata nafasi ya kufika na kufanya kitu hapa Tanzania, ameongea na EATV kuhusiana na ziara yake hapa Tanzania, ambapo amesema anafurahi sana kupata nafasi hii, na kutokana na uwepo wake anaamini kuna kitu cha tofauti ambacho kitatokea hususan siku ya leo.

Msanii huyu ambaye kwa sasa ana albam kali kabisa mbili, My Praise, na All Praise, amesema kuwa kwa sasa yupo katika matayarisho ya albam yake ya 3 itakayokwenda kwa jina la Glory, na katika mahojiano yetu, akatoa ushauri kwa wasanii wa Tanzania kuhusiana na siri ya kufanya vizuri katika soko la kimataifa ambapo amewataka wasanii hawa kujitengeneza wenyewe binafsi katika njia za kisanii na kufanya kazi nzuri ambazo zitawasaidia kupiga hatua na kuvuka mipaka kwa kazi zao.