Tuesday , 18th Mar , 2014

J Martins, mwanamuziki kutoka nchini Nigeria ambaye amekuwa huko Liberia hivi karibuni kwa ajili ya mishe za kimuziki amesema kuwa, ameona vipaji kibao ndani ya nchi hiyo ambavyo vinaweza kutikisa chati za muziki kimataifa.

J Martins ambaye amejipanga kuanza kufanya kolabo na nyota wa nchi hiyo amesema kuwa, tayari mipango imekwishaanza ya yeye kurekodi kazi na msanii Tarkun J ambaye tangu ametua huko Liberia amekuwa akisikia sifa zake kibao kila kona ya nchi hiyo.

J Martins amekuwa katika Jiji la Monrovia kwa ajili ya shughuli kubwa ya shoo ya muziki ambapo amesisitiza kuwa, kwa vipaji ambavyo ameona nchini humo, anastahili kuwa na kazi kubwa ya kufanya
kuvitangaza vipaji hivi ili kuvipatia nafasi ya kusikika katika jukwaa la Kimataifa.