Saturday , 7th Jun , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Jaguar amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, kazi yake mpya baada ya ngoma ya Kioo inayofanya poa kwa sasa, ipo tayari ikiwa na dalili zote za kuachiwa hivi karibuni.

Jaguar

Jaguar ambaye hajatoa taarifa zaidi juu ya kazi hii amesema kuwa, binafsi ametokea kuikubali sana kazi hii, baada ya kusikiliza ikiwa imekwishafanyiwa 'Mastering' na kuona kuwa ipo katika kiwango cha kuwarusha tena mashabiki wake.

Kwa sasa msanii huyu anasikiliziwa kwa hamu kubwa kutangaza rasmi ni lini atawapatia mashabiki kazi hii mpya hasa kutokana na mlolongo wa kazi zake kuonesha ubora wa hali ya juu kila siku.