Monday , 4th May , 2015

Diva wa muziki Jackie Chandiru hatimaye imedhihirika kuwa amefunga ndoa, katika sherehe ya kimyakimya iliyofanyika nchini Uganda na kualika baadhi ya wanafamilia na marafiki wa karibu sana.

msanii wa muziki wa Uganda akiwa na mumewe Nal Van Vliet

Msanii huyo wa muziki ambaye ngoma yake ya Goal Digger ndiyo iliyomuweka sawa katika game ya muziki, amefunga ndoa na mchumba wake mwenye asili ya ki -Polish, Nal Van Vliet.

Msanii huyo amejisikia sifa kubwa ya kuweka maisha yake binafsi pembeni ya kazi zake za muziki kwa miaka mingi sasa, kwa hatua hii amewapatia majibu wengi waliokuwa wakihisi huenda ana mahusiano na msanii wa muziki, Alaka.