Monday , 2nd Feb , 2015

Star wa muziki Iyanya kutoka Nigeria ameibuka na kujibu mashambulizi ya tuhuma za kutokutoa ushirikiano kuitangaza video ya kolabo aliyofanya na msanii Jaguar wa Kenya.

Wasanii Iyanya wa Nigeria akiwa na Jaguar kutoka nchini Kenya

Iyanya amesema kuwa asingeweza kufanya kazi ya msanii huyo bila kuona jitihada zake binafsi kujitangaza huko Nigeria.

Iyanya kwa mtazamo wake amesema kuwa, Jaguar alitakiwa kufanya harakati za kujitangaza kwanza Nigeria kwa mahojiano na vituo vya huko, ushauri ambao anadai kuwa alimpatia msanii Diamond Plantumz na Sauti Sol pia.

Wiki kadhaa zilizopita Jaguar alisimama katika jukwaa na kusema wazi kuwa, Yeye na msanii Iyanya licha ya kufanya kolabo, haziivi tena hasa baada ya star huyo kukataa kuisambaza video ya kolabo yao ya One Centimetre remix huko Nigeria, kitendo kinachoonesha chuki ya waNigeria kwa muziki wa Afrika Mashariki.