Saturday , 17th May , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Iryn Namubiru ameibuka na malalamiko kwa wadau wa muziki Uganda, hususan Ma-DJ's ambao wamekuwa wakitumia kazi zake kwaajili ya kujinufaisha bila kuwasiliana naye kuweka makubaliano.

Iryn Namubiru

Iryn amesema kuwa, inasikitisha sana kuona kuwa anawekeza nguvu na pesa nyingi kutengeneza rekodi ambazo baada ya kukamilik, huchukuliwa na watu, kusambazwa na kutengenezewa remix za mixing zinazouzwa bila yeye kuona faida yoyote.

Iryn amesema kuwa, hiki ni kilio cha wasanii wengi, isipokuwa wanaogopa kusema kwa kuhofia kazi zao kuacha kupigwa , na amewataka wadau hawa wa muziki kufahamu juu ya kilio hiki na kuacha unyonyaji wanaofanya.