Wednesday , 22nd Mar , 2017

Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi, Harmonize amefunguka na kudai alipata hofu ya kufanyiwa fitina kwenye muziki baada ya uongozi wake kumtaka kuachia wimbo wake mpya kupitia mtandao ulioanzishwa na lebo hiyo.

Harmonize

Harmonize amefunguka katika Planet Bongo na kusema kuwa uongozi wake ulipomtaka kumtanguliza kama chambo alidhani wamedhamiria kumpoteza katika ramani ya muziki ndiyo maana hawakutaka kuutambulisha wenye radio na televisheni kitu ambacho kimezoeleka.

"Unajua mimi WCB ni kama chambo kwa sababu hata lebo ilipoanzishwa mimi ndiye niliyekuwa msanii wa kwanza kusaini na nikafanya vizuri wengine wakaja, hata hivyo kwenye mauzo ya muziki kwenye mtandao nimetangulizwa mimi na namshukuru Mungu kazi zimepokelewa vizuri. Uongozi ulikuwa na mtazamo chanya tofauti na nilivyowaza." alisema Harmonize.

Aidha masanii huyo amesema baada ya kiongozi wa lebo hiyo Diamond Platnumz kutoa albam yeye atauomba uongozi wake pia afanye hivyo kwani aliaibika alipofika Marekani alipoulizwa ana albam ngapi kama msanii akakosa jibu.

"Nadhani Mondi akishamaliza suala la Albamu mimi nitafuata kwa sababu nilipokuwa Texas kuna mdada nilimuambia mimi ni msanii kutoka Tanzania akaniuliza mpaka sasa una albamu ngapi nikashindwa kumjibi, hii ni aibu ukiwa na albamu kadhaa lazima watu wakuheshimu" aliongeza Harmonize