Friday , 31st Mar , 2017

Msanii kutoka Chafu Pozi lebo ya LFLG anayetamba na hit song ya Mazoea, Billnass ameonesha asivyo msahaulifu wa fadhila kwa kumshukuru mwanamuziki Naazizi kutoka kundi la Necessary Noise kutoka Kenya na kumtaja kuwa ndiye aliyemfanya ang'are.

Naazizi, Billnass

Billnass akimpongeza Naazizi kwenye siku yake ya kuzaliwa wiki hii, ameeleza kwamba chorus iliyofanywa na mwanadada huyo kwa ushirikiano na TID katika  'hit song' ya 'Raha' ndiyo iliyomtambulisha kwenye game ya bongo fleva na kumuweka juu hadi leo kutokana na love na uwezo aliouonesha.

“U know I love u have a blast chorus yako ndo imefanya leo wananiita Nenga mara Mzungu Mzee nabado nakomaa tu hope ur very proud too hbd , ...Nakutakia maisha marefu miaka mobb momma wa taifa"  Aliandika Bill nass

'Story' za mwanzo kabla ya Naazizi kutua Bongo na kufanya chorus yake na Billnass mipango ya TID ilikuwa ni kukaa mwenyewe katika kiitikio cha wimbo huo wa 'Raha' ambao ulifanywa katika studio za defatality Music ya Mensen Selekta.