Monday , 24th Aug , 2015

Akiwa anafanya vyema na wimbo wake 'Imebaki Story' msanii wa muziki ambaye pia ni muigizaji nyota wa filamu wa nchini Tanzania Hemed PHD hivi sasa ameamua kumpa shavu msanii Mr Blue katika ngoma mpya inayosukwa hivi karibuni.

Msanii wa muziki ambaye pia ni muigizaji nyota wa filamu nchini Tanzania Hemed PHD

Hemedi ameongea na eNewz na kusema kuwa anamfagilia sana mkali huyo na hivi sasa atashiriki naye katika wimbo mpya unaoitwa 'Someday' ambao upo jikoni, huku akielezea zaidi mipango yake katika muziki kwa sasa kutokana na kujitegemea yeye binafsi katika kukuza kazi zake bila menejiment yeyote ile.