Friday , 7th Aug , 2015

Kundi la muziki la H_Art The Band kutoka Kenya, baada kujivunia mafanikio makubwa katika muziki, limeanza kufaidi matunda ya ustaa wao baada ya kupata shavu la kuwa mabalozi wa bidhaa mpya ya chakula Kenya.

Kundi la muziki la H_art band la nchini Kenya

H_Art ambao wamejijengea umaarufu kupitia rekodi zao kama vile Uliza Kiatu na Nikikutazama, hawajaweka wazi bado juu ya kitita walichoingiza kutoka katika dili hiyo, ila inakuwa ni mwanzo mzuri wa safari yao kuelekea katika kilele cha mafanikio kimuziki.

Bendi hiyo kwa sasa ipo katika kutangaza rekodi yao mpya inayokwenda kwa jina Baby Love, wakiendeleza mtindo wao wa kuenzi utamaduni wa Kiafrika katika muziki mpaka muonekano wao.