Friday , 6th Nov , 2015

Msanii aliye chini ya lebo ya WCB Harmonize amethibitisha kuwa video yake ya Aiyola inatarajia kutoka rasmi leo na EATV ndio itakuwa ya kwanza kuonyesha video hiyo.

Harmonize amefunguka juu ya hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba anatimiza ahadi yake aliyowaahidi mashabiki wake kuwa video hiyo itakapokuwa tayari atawajulisha mara moja.

"Niliahidi katika Planet Bongo kuwa siku ya kutoa video ikishafika nitawaambia Watanzania wote na Wanamashariki kwa ujumla kuwa video inatoka, naomba nitimize ahadi yangu kuwaambia Watanzania wote amabao mnasikiliza Plane Bongo ya East Africa Radio muda huu, kuwa video ya Aiyola inatoka rasmi leo, na tukutane baadae kwenye FNL ya East Africa Tv", alisema Harmonize.

Video hiyo ya Harmonize imetengenezwa nchini Afrika Kusini, na ndiyo video yake ya kwanza kufanya chini ya WCB.