Tuesday , 27th Jan , 2015

Msanii Frasha kutoka kundi la P Unit, amefafanua hatua yake ya kuamua kufanya project zake nje ya kundi na kusema kuwa huo ni mkakati wa kujitengenezea jina binafsi ambalo litasaidia kusongesha biashara zake nyingine nje ya shughuli za Kundi.

Msanii wa kundi la P-Unit wa nchini Kenya Frasha

Frasha ameweka wazi kuwa, project hiyo binafsi ameipatia jina "I am Frasha", na ndani yake itakuwa ikijihusisha na kusimamia wasanii, matangazo, utayarishaji video na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo.

Kwa wale mashabiki wenye wasiwasi kuhusu uwepo wa kundi la P Unit, rapa huyu amewahakikishia kuwa hakuna mpango wala dalili yoyote ya kuvunjika kwa kundi hili ambalo litaendelea kufanya kazi zake kama kawaida.