Wednesday , 6th Jan , 2016

Picha ya awali ya mwigizaji Lupita Nyong'o kutoka katika filamu aliyoigiza huko nchini Uganda, The Queen of Katwe zimeachiwa rasmi na timu ya utayarishaji kazi hiyo kutoka Disney hadharani.

mwigizaji nyota wa nchini Kenya Lupita Nyong'o

Kuachiwa huko rasmi kwa filamu hiyo ni kama matayarisho ya awali kuelekea kuachiwa kwa kazi baada ya kumalizika kwa msimu wa kiangazi mwaka huu.

Filamu hiyo inayongojewa kwa hamu kwa mujibu wa Lupita, inahusiana na kujikita katika kusimamia ndoto, akiweka wazi kuwa makazi duni ya huko Katwe Uganda ni sehemu ngumu kabisa ambayo licha ya mazingira yake, wakazi wake wanaendelea kuishi kwa heshima na kuendeleza shughuli zao za siku hadi siku.

Kuelekea ujio wa kazi hiyo unaotanguliwa na picha hiyo maalum, Lupita ameeleza kuwa ushiriki wake anauchukulia kama kurudi nyumbani, kutokana na asili yake ya Afrika Mashariki, Uganda ikiwa karibu kabisa na taifa la asili yake la Kenya.