Monday , 18th Dec , 2017

Muimbaji na Mtayaishaji wa nyimbo za injili Fidel Ombeni ambaye mwaka 2015 alitoa wimbo wake uliojulikana kwa jina la ‘Nani kama Yesu’ na kujizolea umaarufu nchini na sehemu tofauti duniani,

kwa sasa anarudi tena na wimbo mpya kwaajili ya kufungia mwaka 2017.

Akizungumza na mwandishi wa EATV Digital, Fidel Ombeni ambaye kwasasa anaishi na kufanya shughuli zake za muziki nchini Norway, amesema kabla ya mwaka huu haujaisha atatoa wimbo mpya utakaojulikana kwa jina la ‘Mpenzi’

“Ninayo furaha kubwa sana ndani ya moyo wangu kuwajulisha wapenzi wote wa muziki wangu ya kwamba kabla mwezi huu wa Desemba hauja isha, kuna kibao kipya kipo njiani kinachoitwa MPENZI na ninaamini kila mmoja atakayesikiliza wimbo huo atabarikiwa kwa namna ya pekee sana”. Amesema Fidel

Kabla ya wimbo huu anaotaka kuachia mwezi huu wa Desemba, wimbo wake wa mwisho aliochia ulikuwa unajulikana kwa jina na ‘Yesu ni njia’, utazame hapo chini.