Monday , 29th Dec , 2014

Akiwa ni mmoja wa wakongwe katika gemu ya muziki wa Bongofleva nchini msanii Abdul Sykes 'Dully Sykes' amejipanga kusheherekea miaka 15 ya muziki wake tangu alipoanza kutamba katika gemu ya muziki.

Msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Dully Sykes

Dully Sykes ameelezea kuwa katika kipindi chake chote tangu ameanza muziki amefanya mengi mazuri akiweka wazi kuwa kuna wasanii ambao wamepotea katika gemu na wengine walikata tamaa kutokana na ugumu wa soko.

Dully amesema kuwa kutokana na changamoto zote alizopitia anatarajia kesho kuungana na wasanii mbalimbali jijini DSM wakiwemo Barnaba, Linnah, Vee Money, Makomandoo, Ommy Dimpoz na wengineo wengi katika kusheherekea miaka 15 ya muziki wake na kuufungua mwaka mpya kwa kazi mpya.