Friday , 11th Apr , 2014

Staa wa muziki kutoka Jamaica, Collins Demar Eadwards maarufu zaidi kama Demarco ambaye
anatarajia kutua nchini Uganda kwaajili ya onyesho mwezi Mei, anatarajia kutumia nafasi hii pia kufanya kolabo kadhaa na mastaa wa muziki kutoka nchini humo.

Demarco

Demarco ambaye amekwishafanya kazi yenye mafanikio na msanii Peter Miles, atatumbuiza katika tamasha la Street Jam, akiwa na sapoti kutoka kwa wasanii Chameleone, Mun G, Vampino na wengine ambapo kutoka orodha hii, wasanii hawa wapo katika nafasi kubwa kuwepo katika orodha ya kolabo alizopanga kufanya staa huyu wa kimataifa.

Ujio wa Demarco Afrika Mashariki, unafuata ujio mwingine mkubwa wa staa kutoka Jamaica, Konshens ambaye sasa yupo huko Kenya kwaajili ya onyesho kubwa la muziki litakalofanyika hapo Kesho.

Tags: