
Dudubaya
Akizungumza katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV, Dudubaya amesema msanii mwenzake Chid Benz na wasanii wengine hawawezi kuacha kutumia madawa ya kulevya kwa watu kuwapeleka popote kama dhamira yao haijawasuta kuhusu jambo hilo.
“Kama una mtoto ambaye ni changudoa hata ufanye nini kama dhamira yake haijamsuta akaamua kwa dhati kutoka moyoni mwake hataacha atakuwa anaruka hadi ukuta ndivyo ilivyo kwa watu ambao wameshajiingiza kwenye madawa ya kulevya” Amesema Dudu Baya.