Monday , 8th Sep , 2014

Mwigizaji maarufu kutoka Nigeria, Desmond Elliot amekuwa nchini Kenya kwa ajili ya kazi ya kupiga picha za tamthilia mpya ambayo inabeba visa mbalimbali vya kumulika masuala ya siasa na rushwa katika jamii.

Muigizaji wa filamu wa Nigeria Desmond Elliot

Kazi hii yenye kiwango cha kimataifa imekuwa ikifanyika huko Muthaiga ambapo ndipo yalipo mandhari sahihi ya maudhui ya kazi hii ambayo inatarajia kuwa na msisimko wa aina yake pindi itakapokamilika.

Desmond katika kazi hii anashirikiana na waigizaji wengine mahiri kutoka nchini Kenya, akiwepo Gerald Langiri katika orodha hiyo.