Friday , 31st Oct , 2014

Msanii wa muziki Desire Luzinda, amepata misukosuko baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kutokana na kudaiwa deni la shilingi milioni 21 za Uganda alizokuwa amemkopa Peter Mugwanya.

Msanii huyu alikamatwa akiwa katika mizunguko yake ya kawaida huko jijini Kampala, na kufanikiwa kuachiwa baada ya kupata msaada wa kiasi cha pesa, shilingi milioni 10 kutoka kwa rafiki yake Ntenge Sssebagala ambaye alitoa shilingi milioni 10 kusaidia kupunguza deni hili.

Desire ambaye haikufahamika mara moja kuwa alikuwa amekopa kiasi hiki cha pesa kwa matumizi gani, ambapo imeelezwa kuwa amepatiwa mpaka tarehe 30 mwezi Novemba kumalizia kiasi cha pesa ambacho alikuwa anadaiwa.