Monday , 20th Apr , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Desire Luzinda, ameonekana kujiweka karibu kabisa na dini ameweka mpango wake wa kutoka na rekodi ya kidini, baada ya kushuhudia mambo makubwa kabisa Mungu aliyomtendea.

msanii wa muziki wa Uganda Desire Luzinda

Desire ambaye kufuatia hatua yake hii tayari amezua mitazamo tofauti kutoka kwa mashabiki wake, lakini amewataka watu kufahamu kuwa, kuna nguvu kubwa katika ulimi wake, na kuwataka kuwa makini na kile wanachokisema na kukaa tayari kwa rekodi hiyo kali.

Desire anakuwa si msanii wa kwanza kufanya hatua kama hiyo kutoka Uganda, ambapo tayari msanii Bebe Cool, Jose Chameleone, Juliana Kanyomozi na Grace Nakimera wamekwishafanya ngoma za aina hiyo.