Tuesday , 22nd Apr , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Dezire Luzinda ameinga katika mtihani hasa baada ya tamasha lake kubwa la Black and White Affair alilopanga kulifanya mwezi wa 6, kukosa madhamini yoyote mpaka sasa na kumpatia changamoto ya kugharamia onyesho hilo.

Desire Luzinda

Dezire ametajwa kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 12 za Uganda na bendi hii, pesa ambazo anasita kuzitoa katika mfuko wake mwenyewe kwa kuhofia hasara endapo onyesho lenyewe litabuma.

Imeelezwa kuwa, kwa sasa msanii huyu anatafuta njia za kuweka mambo sawa ili asishushe hadhi yake kupitia onyesho hili ambalo linakuwa ni kubwa kabisa na la binafsi kwake kuandaa kama msanii anayejitegemea.