Wednesday , 24th Jun , 2015

Star mkongwe wa gemu ya rhumba na dansi, Deo Mwanambilimbi ametoa tathmini yake ya muelekeo wa muziki wa dansi katika kipindi cha sasa, akidai kuwa ushabiki umepungua kwa upande huo, wakibanwa sana na vijana wanaofanya miondoko ya Bongofleva.

Deo Mwanambilimbi

Hata hivyo staa huyo ambaye amekuwa ni adimu sana kuonekana katika vyombo vya habari, amedai kuwa ladha ya dansi inarudishwa na kizazi kipya, akitaka pia wasanii wa zamani kubadilika na kuchanganya ladha za kisasa katika rhumba na dansi kupata mashabiki vijana pia.

Msanii huyo ambaye pia ameahidi kutoka na nyimbo mbili sambamba na video zake kabla ya mwaka kuisha, amesema kuwa anavutiwa na jitihada za sasa za wasanii wa kizazi kipya wakiwepo Yamoto Band kurudi katika muziki wa Live na kutumia vionjo vya dansi zaidi.