Saturday , 10th May , 2014

Msanii wa muziki Demarco, tayari ametua nchini Uganda kwa ajili ya onesho lake ambalo litafanyika leo, ambapo katika mkutano wake na waandishi wa habari, ameweka wazi kuwa wasanii wa nchi hiyo anaowaelewa ni Chameleone pamoja na Peter Miles.

Demarco

Demarco amesema kuwa, katika wakati ambapo amekuwa huko Uganda, wasanii anaowasikia na kuwakubali ni hawa wawili tu, kauli ambayo imewashangaza na kuwahuzunisha wengi hususan kutokana na kuwepo kwa wasanii wengi wa nchi hiyo wanaofanya vizuri hasa katika miondoko ya dancehall.

Demarco anatarajiwa kudondosha onesho la aina yake leo hii huko Uganda, hasa kutokana na yeye na timu yake kutumia muda mrefu kujipanga kwaajili ya tukio hili kubwa.

Tags: