Tuesday , 27th Jan , 2015

Baada ya kufungua mwaka na ngoma mpya inayokwenda kwa jina Tunaishi aliyomshirikisha star Ney wa Mitego, Rapa Darasa amesema kuwa ameifanya kazi hii baada ya kujipa muda kutafakari nafasi yake katika game na kugundua mapungufu yake.

Msanii wa miondoko ya bongo fleva nchini, Darasa

Darasa amejitaja kama rapa ambaye mashabiki wake walimuamini ndani ya kipindi kifupi na yeye kugundua kuwa kuna sehemu hakuwatendea haki, na hivyo rekodi yake mpya ya Tunaishi inakuwa ni kazi ambayo anaamini inatoa majibu na kumrudisha katika nafasi yake kimuziki.