Sunday , 6th Jul , 2014

Mwanamuziki Elidaima Chikira aka Daima wa nchini Tanzania mwenye makazi yake mjini Tokyo nchini Japan amanzisha bendi yake aliyoibatiza jina 'Press The Seal' inayotamba na vibao vyake viwili vilivyobatizwa jina 'This is life' na 'Gwaride'.

Mwanamuziki Daima akiwa na Dk. Ghalib Bilal nchini Japan

Daima ameiambia eNewz kuwa ndani ya bendi yake hiyo mpya inayotumbuiza sehemu mbalimbali jijini humo, ina wanamuziki wazungu wawili, Mjapan mmoja na Mcarebeani mmoja huku yeye mwenyewe akiwa ndie vocalist.

Daima ambaye ni mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Reggae, Hard Hip Hop Soul na miondoko mingine mingi, ni muandaaji pia wa maonyesho makubwa ya matamasha ya muziki wa live na amekuwa akiwaalika watumbuizaji nyota kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo Nigeria na pia nchini Japan.

Kwa kifupi tu Daima ni mzaliwa wa mjini Dodoma ambaye familia yake ipo mkoani Mororgoro, ambapo hivi sasa amefunga ndoa na mke wake raia wa nchi hiyo aliyezaa nae mtoto mmoja wa kike.