Saturday , 4th Jul , 2015

Msanii Colonel Moustapha kutoka nchini Kenya, ametoa kauli tata kuhusiana na vita ya maneno kati yake na Nyota Ndogo kuhusiana na suala la maadili, ambapo Colonel ameeleza kuwa Nyota Ndogo amekuwa akimtaka japo hana ujasiri wa kuliweka hilo wazi.

Colonel Moustapha

Colonel ameeleza kuwa, kushambuliana kwa maneno sana na Nyota Ndogo kumepelekea mashabiki wao kuhisi pengine waliwahi kutoka pamoja kipindi cha nyuma, kitu ambacho alisema hana maelezo juu yake isipokuwa tu, ukweli kuwa aliwahi kukutana na Nyota Ndogo na kubadilishana namba za simu.

Nyota Ndogo kwa sasa yuko nchini Ujerumani na mpenzi wake, na tayari amekwishakanusha kuwahi kuwepo kwa mahusiano yoyote ya kimapenzi na Moustapha.

Nyota Ndogo