Wednesday , 28th May , 2014

Staa wa muziki Kenya, Colonel Moustapha, baada ya skendo za mahusiano katika kipindi cha hivi karibuni, kwa sasa ameibuka kivingine ambapo taarifa zinaweka wazi kuwa yupo katika mpango wa kurudi shule kujiendeleza kimasomo.

Colonel Moustapha

Endapo mambo yatakwenda sawa, Colonel Moustapha atajiunga na Chuo Kikuu cha Mount Kenya kwa ajili ya kuchukua shahada katika fani ya usimamizi wa biashara, fani ambayo anaamini itamuwezesha kuendesha shughuli zake za muziki vizuri.

Colonel Moustapha amekiri kuwa, katika kipindi cha awali hakuwa anachukulia shule katika uzito wake kutokana na maswala ya muziki ingawa sasa amepata mtazamo mpya.