Friday , 16th May , 2014

Msanii wa nchini Rwanda, Aisha Uwimana maarufu zaidi kama Ciney ameendelea kupiga hatua katika muziki wake na safari hii amefanikiwa kupata shavu la mkataba wa miaka mitatu chini ya Record Label kubwa ambayo inakwenda kwa jina Infinity.

Ciney

Msanii huyu tayari amekwishafanya rekodi 3 chini ya lebo hii, huku akiwaahidi mashabiki zake kazi nyingine kali zikiwemo kolabo na wasanii wakubwa wanaofanya vizuri katika game ya muziki Rwanda.

Ciney amejijengea umaarufu mkubwa kupitia kazi yake inayokwenda kwa jina Game of Love, akiwa amejipanga kuachia video ya kazi yake ya kwanza chini ya Infinity, ya rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina Salam.