Thursday , 5th Jun , 2014

Wasanii wa nchini Uganda, Moze Radio, Weasel pamoja na Chameleone baada ya kumaliza ziara zao nje ya Uganda, wameamua kujichimbia studio kwa ajili ya kutengeneza kazi ya pamoja.

Jose Chameleone, Radio na Weasel

Hatua hii ya wasanii hawa kuamua kukutana na kufanya kazi kwa pamoja, imeonesha moyo wao mkubwa katika shughuli ya muziki licha ya misukosuko na ugomvi ambao wamekuwa wanakabiliana nao, hasa kwa upande wa Moze Radio na Weasel katika siku za karibuni.

Muunganiko katika kazi moja kwa mastaa hawa ambao kwa muda mrefu hawakuwa na maelewano, ni moja kati ya vitu ambavyo mashabiki wa muziki Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla wamekuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kwa simu nyingi sasa.