Saturday , 6th Dec , 2014

Mrembo aliyekuwa anashikilia taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2012, Brigitte Alfred ameendelea na jitihada za kuisaidia jamii kupitia taasisi yake ya BAF ama Brigitte Alfred Foundation.

Brigitte Alfed - Miss Tanzania 2012

Mrembo aliyekuwa anashikilia taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2012, Brigitte Alfred ameendelea na jitihada za kuisaidia jamii kupitia taasisi yake ya BAF ama Brigitte Alfred Foundation ambayo mpaka sasa imekwishafanikiwa kuwapatia mafunzo vijana wapatao 50, kuwawezesha kujitegemea na kuwa na manufaa katika jamii.

Brigitte amesema kuwa, anaendeleza jitihada hizi baada ya kufanikiwa kufika nafasi ya juu Miss World katika shidano la Beauty With A Purpose, akiwa na malengo ya kuendelea kutumia nafasi, uwezo na urembo wake kuleta mabadiliko chanya kwa vijana hususan wale wenye ulemavu wa ngozi.

Kabla hatujaagana pia, Mrembo huyu alikuwa akitumia nafasi ya mahojiano yetu naye kumtakia mrembo Happyness Watimwanywa kila la heri akiwa huko London kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World.