Monday , 16th Mar , 2015

Msanii wa muziki Bobi Wine ameachia rekodi yake ya kwanza kabisa kufanya kwa lugha ya Kiswahili, aliyoipatia jina Paradiso, kazi ambayo kwa mujibu wake ameifanya ikiwa ni ushauri kutoka kwa marehemu baba yake.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Bobi Wine

Staa huyo amesema kuwa, hakuufanyia kazi ushauri huo kwa muda kutokana na kuepusha kuonekana kuwa anamuiga msanii wa muziki Jose Chameleone ambaye rekodi zake nyingi uhusisha Kiswahili, hasa ikizingatiwa pia hakuwa na maelewano mazuri naye.

Staa huyo ambaye hivi karibuni amempoteza baba yake mzazi, amesema kuwa ingawa amekamilisha kazi hiyo baada ya baba yake kufariki, anaamini kuwa huko alipo Paradiso, anaisikiliza na kutabasamu.