Friday , 3rd Jul , 2015

Star wa muziki Belle 9 ambaye ana kundi kubwa la mashabiki nyuma yake wanaofikiri kuwa bado hajaitendea haki ushindani uliopo katika game ya Bongo Flava kwa sasa, amejitapa kujitengenezea nafasi ya aina yake kwa kazi kali zaidi mwaka huu.

msanii wa miondoko ya bongo fleva nchini

Ni takribani miaka 8 sasa belle 9 amekuwa akitoa kazi nzuri ambazo zimemuwezesha kuendelea kusikika.

Mkali huyo ameiambia eNewz kuwa, hakuna msanii mwingine ambaye ameweza kutengeneza nafasi ambayo yeye amejitengenezea kwa sasa, akieleza kuwa amekuwa mwaminifu miaka yote kuhakikisha kuwa kazi zake mpya zinazidi kwa kiwango kama zile zilizotangulia.