Friday , 4th Dec , 2015

Nyota wa muziki Belle 9 ambaye anaweka rekodi ya kuzigusa anga za kimataifa kupitia kazi ambazo zimesukwa ndani ya mipaka ya nchi tofauti na wasanii wengine, ikiwepo kazi yake mpya ya Burger Movie Selfie itakayotoka wiki ijayo.

Nyota wa muziki Belle 9

Katika kuliweka wazi zaidi mkali huyo amesema hatua hizo ni kutokana na kuanza kufanya kazi chini ya uongozi, Vitamin Music.

Belle 9 amesema kuwa, sambamba na hilo ubora, mabadiliko na hatua kubwa kama hizi alizofikia sasa, ni kutokana na kuamini katika kile anachofanya, kauli hii ikiwa pia ni kama ushauri kwa wasanii wanaochipukia.