Thursday , 1st Oct , 2015

Star wa muziki Christian Bella ambaye ni raia wa DRC anayeendesha shughuli zake za muziki hapa Tanzania, amesema kuwa anaiombea Tanzania kudumisha amani yake katika kipindi hiki na kuvuka uchaguzi kwa usalama.

Staa wa muziki wa miondoko ya dansi nchini Christian Bella

Star huyo anayemiliki bendi ya 'Malaika Music Band' amesihi wananchi kuepuka kuteleza kutokana na mifano dhahiri ya kuibuka kwa fujo katika baadhi ya nchi duniani katika kipindi kama hiki.

Bella ameeleza kuwa, kwa upande wake binafsi hafahamu sana siasa, akiwa kama moja wa raia wa kigeni anaelewa dhahiri kuwa sifa kubwa ya Tanzania ni amani ambayo kuna kila sababu ya kuendelea kuitunza, siri pekee ikiwa ni kila mtu kwa nafasi yake kupima wagombea, kuamua ni nani wanamuhitaji na kupiga kura bila kukosa.