CHRISTIAN BELLA
Akiongea ndani ya eNewz Bella amesema 'Haruhusiwi msanii wa Malaika Band kutoa wimbo bila idhini yangu, na inakuaje msanii wangu anatoa ngoma mbili lakini hata hazisikiki, Hii inanitia aibu”.
Bella aliongeza “Lakini pia alikuwa anataka ustaa kama Christiani, nikinunua gari na yeye anataka anunue”.
Hata hivyo Bella alikanusha stori kuwa huwa anaacha kila kitu anachokitumia bongo yaaani mpaka simu anapokwenda kwa mama watoto wake ili kulinda mahusiano yake na mke wake. Na kusema yeye si mtu wa michepuko.




