Tuesday , 23rd Sep , 2014

Msanii wa muziki Bebe Cool ametakiwa kuwaomba radhi watu wa Sudan Kusini, kutokana na hatua yake ya kutangaza kuwazuia kushiriki katika shughuli zake zozote za muziki.

msanii wa nchini Uganda Bebe Cool

Hii ni baada ya serikali hiyo kutishia kuwaondoa raia wote wa kigeni katika sekta zao za kiuchumi.

Bebo Cool kwa kauli yake, ameonekana kama mchochezi mwenye nia ya kubomoa zaidi mahusiano mema na kujenga uadui kati ya watu kutokana na migongano ya kisiasa, akiwa kama msanii mwenye ushawishi mkubwa.

Kati ya watu mashuhuri waliomtaka Bebe Cool aombe radhi kwa wa-Sudan Kusini kwa kauli hii, ni pamoja na hasimu wake Bobi Wine ambaye ametoa muda wa wiki moja kwa Bebe Cool kukamilisha hili.