Msanii wa Bongo Flava Nay wa Mitego
BASATA ikatumia wasaa huo kuwakumbusha wasanii wote nchini kufanya kazi kufuatana na taratibu zilizopo lakini pia kuangalia maadali ya nchi ili kuhakikisha kuwa mikwaruzano isiyokuwa yalazima inaepukika na kunakua na ushirikiano wa kuinua tasnia nzima ya sanaa nchini.
Kufuatia hali hiyo kipindi cha burudani PLANET BONGO kinachorushwa na E ast Africa Radio kikaueleza umma na mashabiki wa burudani kuhu uamuzi huo wa BASATA ambapo mashabiki wamepewa nafasi ya kuelezea kama wanaridhishwa na hatua ya kuufungia .
Mashabiki wengi ambao wameshiriki swali ‘Unadhani hatua gani inastahili kwa wasanii watakaokiuka sheria za kufanya sanaa?’ wengi wamesema kutokana na kwamba sasa ni wimbo watatu wa msanii huyo unafungiwa ni wakati wa baraza hilo kuonyesha meno yake zaidi kuliko kuishia kufungia wimbo na kuacha mambo yaendelee.
Baadhi ya maoni ni ambayo yanapatikana kwenye ukurasa wa EA Radio facebook ni kama ifuatavyo: Tomm Kasanula TommKasanula........Toka Wagum tunadum oiiiii mjukuuu......kwa upande wangu me naona adhabu ambayo wanastahili wasanii wanaokiuka sheria za kufanya sanaa
Sharo Mresa Toka 99.6 dodoma mi nafikiri adhabu ndo kitu cha msingi ila tukisema kufungia nyimbo zao bado itakuwa haitoshi coz atafanya tu tena kitu kama icho chamsingi itolewe adhabu ambayo itawafunza zaidi.
James Sitta Tokea pande za mtongani kunduchi dar-es-salaam maoni yangu naona nay apewe adhabu ili kurekebisha makosa yake
Kasbet Chatanda wa iringa wafungwe jela miaka mitatu maana wakilipa faini ataludia tena kwakusema atalipa






