Wednesday , 1st Mar , 2017

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Juma Nature amembariki rapa anayechipukia Harmorapa na kuweza kufanya naye kazi chini ya producer T Touchez, iliyopewa jina la 'Kiboko ya Mabishoo'

Juma Nature (kushoto) akiwa na Harmorapa

Katika kazi hiyo ambayo tayari imeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Harmorapa amewachana baadhi ya mastaa akiwemo dansa  Mose Iyobo, na watu wengine ambao wamekuwa wakim-'diss' kuwa hajui muziki na kusema yeye hajali maneno yao machafu kwani yeye amekuja kutafuta pesa.  

Mbali na Mose Iyobo Harmorapa amechana Jacquline Wolper, Aunty Ezekiel na watu wa WCB

Kwa upande wa Harmorapa jana alisema kuwa kwa sasa wanafanya video ya kazi hiyo na kusema wanategemea video ya ngoma hiyo kutoka siku za karibuni. 

Isikilize hapa...