Akiongea kwenye eNews ya EATV, Dogo Janja amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, isipokuwa hufukia hotelini iwapo ameenda kufanya show, ili kubrand show yake kwa kutoonekana hovyo mitaani ikamshushia thamani.
"Sio kweli kama nafikia hotelini, lazima niende nyumbani, ila nakaa hotelini nabrand show yangu ili watu wasinione hovyo hovyo, ila show ikiisha naenda Nyumbani", alisema Dogo Janja.
Pia Dogo Janja amesema yeye akiwepo mkoani Arusha ambako ndio nyumbani kwao, huwa kama balozi wa nyumba kumi.
"Nikienda Arusha nakuwa kama balozi wa nyumba 10, napita nyumba na nyumba kusalimia, mimi sijatokea familia ya hali ya chini hivyo, dingi yangu yupo anajiweza tu", alisema Dogo Janja.

