
BlackBall
Alicia kwa njia ya mtandao ameshukuru wote waliowezesha kufanikiwa kwa tukio hilo mwishoni mwa wiki, likishuhudia mahudhurio kutoka kwa mastaa wakubwa akiwepo Chris Rock aliyesherehesha, Lenny Kravitz, Wale kati ya wengine, akiwepo pia binti wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, Angel Kagame.
Fedha ambazo zimepatikana katika shughuli hiyo zitatumika katika shughuli mbalimbali ambazo taasisi za Alicia zinashirikiana nazo kutoka mashirika yanayokabiliana na athari za gonjwa la UKIMWI kwa namna mbalimbali hususan kwa watoto katika bara la India na Afrika
