Tuesday , 16th Jun , 2015

Star wa michano Stamina ameweka wazi mapokezi makubwa kabisa ya kazi hiyo, kukiwa tayari na wadau waliojitokeza kutaka kumsapoti kusambaza albam hiyo.

Stamina

Baada ya kufanya uzinduzi wa kishindo wa Albam yake huko Morogoro, Star wa michano Stamina ameweka wazi mapokezi makubwa kabisa ya kazi hiyo, kukiwa tayari na wadau waliojitokeza kutaka kumsapoti kusambaza albam hiyo, hatua ambayo ni dalili nzuri kabisa kwa soko la Albam lililokuwa linafifia Tanzania.

Stamina amesema kuwa, kuna baadhi ya taarifa ambazo hawezi kuziweka wazi kwa sasa kutokana na hatua ambazo bado hazijakamilika kimakubaliano, akiwa sawa na uchaguzi wa kufanya tofauti na wazo lake la awali la kuisambaza kazi hiyo binafsi.