Tuesday , 18th Aug , 2015

Diva mkali wa kundi la muziki la Navy Kenzo Aikal staa wa kike wanaofanya vyema katika gemu ya muziki wa Bongofleva ameelezea kuwa mashabiki wengi wameipokea vizuri truck yao mpya inayoitwa 'Visa' ambayo wamemshirikisha mkali Young Dee.

Diva mkali wa kundi la muziki la Navy Kenzo Aikal

Haikal ameiambia eNewz kuwa traki hiyo ya visa waliona ni vyema kumshirikisha mkali huyo kutokana na kwamba ni kijana mwenzao mwenye kipaji cha muziki na kukubalika sana na mashabiki kutokana na juhudi zake, huku akifafanua zaidi kuhusiana na kuubatiza wimbo huo jina la 'Visa'.