Wednesday , 3rd Dec , 2014

Wasanii wa muziki Aika pamoja na Nahreel wameweka wazi changamoto ambazo wamezipata katika kutengeneza video yao mpya Moyoni, kutokana na jitihada za kuhakikisha kila kitu kinapatikana na kinawakilisha uhalisia.

wasanii Aika na Nahreel wa kundi la Navy Kenzo nchini Tanzania

Aika amesema kuwa, kazi hii ililazimika kufanyika mara mbili kutokana na kufutika mara ya kwanza hivyo kuwalazimu kumtafuta muongozaji mwingine Hanscana kuifanya, na kwa mujibu wa Nahreel hii ni kazi ya pili kutoka katika albam yao mpya.