
Wananchi waliotembelea Maonesho ya sita ya teknolojia ya Madini Geita jana wakisubiri katika banda la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita ili kujiandikisha na kupata huduma za uchunguzi wa saratani na elimu kutoka kwa wataalam wa tiba. Huduma hiyo inayotolewa bila malipo na Hospitali ya Rufaa ya Geita kwa kushirikiana na Kampuni ya Geita Gold Mining Company Limited (GGML), inajumuisha uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa mhandisi wa majengo wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo hicho, jijini Arusha.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ntanga wilayani Ngara Mkoa wa Kagera wakati alipofika kuwasha umeme kwenye kijiji hicho.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, akipokea ripoti ya tathmini ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2022/23 ya Taasisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi hiyo, Dkt. Leonada Mwagike, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Kambarage, Hazina, jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Cheti Awamu ya Nne.