
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa paredi ya tuzo na zawadi kwa askari 54 waliofanya vizuri, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema serikali imewekeza pesa kubwa katika miradi ya kimkakati inayojengwa mkoani humo hivyo ni wajibu wa jeshi la polisi kuzuia wizi wa rasilimali hizo.
Kwa upande wake Kamanada wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema, wanaendelea kudhibiti uhalifu hasa katika miradi ya serikali mkoani humo
"Mh. Mkuu wa mkoa ametoa maelekezo kwetu ambayo tutaenda kuyatekeleza, ametuelekeza kuhusu kulinda watu na Mali zao, na tuangalie miradi hii ya kimkakati jeshi la polisi tunaendelea na mikakati ya kuzuia uhalifu kwenye miradi"
Kwa upande wa wadau wa kupinga ukatili wamelihakikishia jeshi polisi kushirikiana nalo katika kupinga vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa tishio mkoani humo.
'Kwasasa ukatili unapungua kwasababu kama wadau na jeshi la polisi lilivyotuhalika hapa tunahakikisha tunapinga ukatili hata kabla haujatokea'.