Wednesday , 1st Jun , 2016

Mwandaaji wa muziki kutoka Studio za Chedaz Record, Abby Dady, amefunguka na kudai kuwa mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka wake wa kujitangaza na ulikuwa ni mwaka wa hasara kwake.

Mwandaaji wa muziki kutoka Studio za Chedaz Record Abby Dady.

Akizungumza na eNewz Abby dady alisema kuwa katika mwaka mzima wa 2015 alitumia kukuza jina lake kupitia wasanii wa Bongo Fleva akiwa anafanya kazi na baadhi yao kwa malipo madogo ama bure kabisa ili kusaidia kukuza jina lake.

“Lilikuwa ni lengo langu kuhakikisha nafanya kazi ya nyimbo nyingi na wasanii tofauti tofauti mwaka uliopita ili watu wanitambue kwa sababu mimi nilikuwa sijulikani lakini mwaka huu ni mwaka wa kazi kuna mambo mazuri na matamu zaidi yanakuja na nimeshaanza na 'Aje',” alisema Abby Dady.